Jumapili 5 Oktoba 2025 - 15:49
Waaajentina nao wamesimama kuiunga mkono Palestina

Hawza/ Katika siku za hivi karibuni, makundi na mashirika mbalimbali jijini Buenos Aires yamefanya maandamano, redio ya wazi na programu za kitamaduni ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na wakati huo huo kutangaza upinzani wao dhidi ya ushiriki wa washirika wa kimataifa katika mgogoro wa Palestina. Mkusanyiko muhimu zaidi unatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 7 Oktoba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kadri siku ya mkusanyiko mkubwa wa kuunga mkono wananchi wa Palestina tarehe 7 Oktoba inavyokaribia, shughuli mbalimbali zimepangwa siku chache kabla ili sauti za mshikamano na madai mahsusi ziweze kusikika. Kwa siku ya Alhamisi tarehe 25 Septemba, Kamati ya Mshikamano ya Argentina na Watu wa Palestina itafanya redio ya wazi mbele ya Wizara ya Mambo ya Nje (Esmeralda 1212). Shughuli hii, chini ya kaulimbiu isemayo“Sio kwa jina letu”, itapinga mkutano wa Milei na Netanyahu, ikitaka kusitishws uhusiano na utawala wa Israel na kuungwa mkono kwa msafara wa kimataifa “ Sumud”.

Jana, kundi la “Harakati ya kujitolea ya Wapelestina, lilikusanyika mbele ya Obelisco (Uwanja wa Jamhuri) kuonyesha upinzani wao dhidi ya kura ya turufu ya Marekani katika Umoja wa Mataifa na kushindwa kupitishwa kwa azimio la kusitisha mapigano, wakisisitiza kwamba nguvu ya turufu ya nchi chache inapuuza matakwa ya wengi katika maamuzi ya kimataifa.

Vilevile, siku ya Jumamosi tarehe 27 Septemba, makundi kadhaa ya wenyeji, yaliweza “Kukusanyika kwa ajili ya Palestina huko Vicente López”, yameitoa wito wa kukutana saa tano asubuhi (11:00) mbele ya Ikulu ya Rais huko Olivos, ili kuonyesha ishara ya mshikamano.

Mbali na mikusanyiko na maandamano haya, hatua za kivitendo na halisi za kusaidia familia za Kipalestina huko Ghaza pia zinaendelea. Miongoni mwazo ni msaada kwa familia ya Abdullah al-Tayibi, mkazi wa Buenos Aires, ambaye familia yake inahitaji kuhamishwa kuelekea kusini mwa Ukanda wa Ghaza kutokana na mashambulizi makali ya Israel.

Pia kampeni za kijamii kama vile “Bafatan ya Mshikamano na Ghaza”, “Meza kwa ajili ya Palestina”, na “Ndege elfu moja kwa ajili ya Ghaza” zinaendelea, zikitangaza viungo vya (links) vya kuzisaidia moja kwa moja familia za Kipalestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha